SUKA KURAHISISHA USAFIRI

Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Kampuni ya Teksol Limited iliyoko Jijini Dar es salaam imezindua Suka App maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa abiria ambayo itatoa huduma ya kipekee kutokana na mfumo huo namna ulivyotengenezwa na ulivyo rafiki kwa abiria.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa huo SACP Jumanne Murilo, wakati akimuwakilisha IGP Kamilius Wambura amesema kuwa kumekua na madereva wengi kuvunja sheria za barabarani hivyo haitasita kuwachukulia hatua za kisheria 

Aidha, amewata madereva wa Kampuni hiyo  kuwa waadilifu pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Kamanda Murilo amesema kwa kupitia Kampuni zilizopita zinazofanana na Suka App ikiwemo Uba na Bolt miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikilalamikiwa na wateja katika uendeshaji wa Kampuni hizo ni tabia za utendaji wa kazi ikiwemo lugha,mavazi, na heshima ambavyo ni miongoni mwa vitu vilivyojenga au kushusha heshima ya kampuni hizo.

"Katika kutekeleza ajira yenu ipo haja ya kufanya mafunzo na kuelekeza jinsi watu watakavyoendesha kampuni katika kutoa huduma sanjari na kutumia lugha zenye staha wakati wa kuwahudumia watu" amesema Kamishina Murilo

Amesema kampuni zinazotoa huduma ni wadau muhimu sana kwa Jeshi la Polisi na Serikali kwenye masuala ya kiusalama licha ya watu hao kupata kazi wao kama Jeshi wanatarajia kuwa nao karibu sana kama sehemu yao ya tatu ya jicho ya masuala ya kiusalama.

Aidha,ameitaka Kampuni ya Teksol kutoa ajira kwa watu ambao wanamsaada siyo tu kwa faida yao bali kwa faida ya Mkoa wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla.

Kwaupande wake Msimamizi wa mifumo ya Tehama Kampuni ya Teksol Limited Raphael Ndagala, amesema faida za kutumia Suka App ni usalama wa uhakika na bei.

"Kumekuwa na mfumuko wa bei katika kutumia usafiri huu mara bei inaongezeka bila utaratibu maalumu hivyo unapotumia huduma yetu unaweza kufuatilia gharama zako na kujua umetumia kiasi gani, amesema Ndagala.

Amesema suala la usalama tunalizingatia sana kutokana na kuwepo tabia za madereva kutofuata sheria za barabarani hivyo wao kama Suka App wamekuja na utaratibu wa kuhakikisha dereva anaekiuka sheria anawajibishwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria hususani madereva pikipiki na bajaji.

Naye Afisa Leseni kutoka Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Jonathani Kitururu, amesema kupitia kanuni za LATRA za usafiri wa kukodi za mwaka 2020 kanuni ya 18 ndio iayozungumzia Tax mtandao na unatoa mashariti ili Kampuni iweze kutoa huduma ni lazima wasajiliwe.

"Pia kanuni za LATRA zinatoa masharti kadhaa ikiwemo upatikanaji wa mfumo muda wote,kutoa taarifa sahihi kwa wakati pamoja na mtoa huduma aliesajiliwa kutoruhusiwa kutoa huduma kale ambapo leseni yake imemaliza muda wake", amesema Kitururu

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Naibu Kamishina kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alex Katundu, amesema uwepo wa huduma hiyo ni kigezo cha ukuaji wa uchumi ndani ya nchi.

"Kuongezeka kwa wadau wa uwekezaji kama Suka App ni Imani yangu kuwa tutaendelea kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi hatua itakayosaidia kukuza uchumi wetu", amesema Katundu.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI