WEMA APATA UBALOZI HELA BET



Na Fatma Ally, Habari Plus, Dar 

Kampuni ya michezo ya kubashiri Hela Bet imempa ubalozi Msanii wa filamu nchini Wema Isack Sepetu ili aweze kuungaza mchezo huo kupitia kampuni hiyo.

 Aidha kampuni hiyo inaendesha mchezo huo wa kubashiri mtandaoni.

Akizungumza mapema leo  Machi,15 2024,Wema amesema kuwa amefurahi kuwa mwanafamilia mpya kutoka kwenye namba moja ya kampuni ya kubashiri ya michezo.

“Mimi huwaga sifanyi  na kampuni ambayo haiko vizuri lakini kwa kuona hii kampuni ya hela bet inafanya vizuri kwa upande wa michezo mtandaoni nikaona nishirikiane nao ili tuweze kufanya kazi.

"Nina waahidi kufanya kazi bega kwa bega kwa kampuni hii ili kuhakikisha inamfikia kila Mtanzania na pia mimi  nitaanza kubashiri na kwa upande wa timu mimi ni shabiki wa Yanga,"amesema Wema.

Aidha amesema atahakikisha kampuni hiyo inatambulika kila sehemu.

Muwakilishi wa  Hela Bet Jacob Mbuya amesema  kampuni hiyo imekuja kuongeza ushindani juu ya sekta ya Michezo yakubatisha nchini.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI