BATA LA MSITUNI FESTIVAL KUFANYIKA PUGU KAZIMZUMBWI, DC MAGOTI AELEZEA

Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Petro Magoti amewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika tamasha kubwa la Msituni maarufu kama "Bata Msituni Festival" lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia katika kutangaza utalii wa Tanzania.

Aidha, tamasha hilo linatarajia kuwakutanisha watu 3000 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo mpaka sasa nchi tatu zimeshathibitisha kushiriki katika tamasha hilo na nyengine zinajiorodhesha ambapo pamoja na mambo mengine watu wataweza kupata burudani za kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari wilaya ya kisarawe  katika hifadhi ya msitu wa mazingira asilia Pugu  Kazimzumbwi ambao unasimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema  tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa ni la kipekee kwani watanzania watapata fursa ya kukaa katika msitu huo kwa takribani siku sita wakifurahia maisha na mandhari ya msitu huo.

 "Msitu huu hauna wanyama wakali bali una mandhari mazuri sana na wanyama mbalimbali wa kuvutia ikiwemo, panzi mwenye rangi ya bendera ya Taifa, ushoroba na Bwawa la Minaki ambapo watapata fursa ya kuvua samaki, kutembea na mitumbwi ndani ya bwawa, kuweka kempu maalum, kula na kunywa na kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na ngoma za asili ikiwemo ngoma ya vanga ya kizaramo" amesema Dc Magoti.

"Tamasha hili pia litahusisha mama ntilie ambao watapika vyakula mbalimbali, hivyo tunaomba waje wajiandikishe kutakua na mbio za pikipiki, kukimbia Msituni pia kutakuwa na samaki choma, nyama choma, Mihogo pamoja na ngoma za asili yaani hata wewe na mkeo mkija mkataka mchomewe mbuzi mzima mtachomewa halafu kutakuwa na siku ya kupanda Mlima ambapo wahudhuriaji watapata fursa ya kuliona Jiji lote la Dar Es Salaam kwa takribani asilimia 95 kutokea juu ya mlima hapa hapa Kisarawe" amesema DC Magoti.

Aidha, ameongeza uwa tamasha hilo kubwa la Msituni Afrika ya Mashariki linatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani elfu tatu wengi wakiwa ni watalii kutoka nje ya Mipaka ya Tanzania kwa kukaa katika eneo moja na Watanzania kusheherekea utamaduni na uzuri wa asili wa Afrika  na ambapo watakaohudhuria tamasha hilo watapata Kila aina ya burudani wanayoitaka maishani kupitia utalii wa ndani sawa na dhana ya utalii hapa nchini 'Tanzania Unforgetable' yaani Tanzania isiyosahaulika.

Amesema Tamasha hilo litahusisha watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika ya Kusini, Kenya,Uganda huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa shughuli hiyo ambayo itafanyika ndani ya hifadhi ya msitu wa asili,Pugu Kazimzumbwi ambapo kiingilio cha juu kitakuwa shilingi laki moja na nusu 15,0000 kwa watanzania kwa siku zote nne watakazokuwa ndani ya msitu huo, kwa wageni laki 250000.

Kwa upande wake, Afisa Mhifadhi wa wilaya ya Kisarawe kutoka wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) ambaye pia ni Meneja  wa hifadhi hiyo ya msitu  asili,Pugu-Kazimzumbwi Baraka Mtemwa amewakaribisha watanzania kutembelea hifadhi hiyo kwani watajionea vitu mbalimbali ikiwemo miti, ndege panzi mwenye rangi za bendera ya Taifa la Tanzani,Ushoroba na Bwawa la Minaki,huku akisisitiza pia huduma ya malazi kwenye mazingira ya msitu huo pia inapatika na wamejipanga vyema kuwahudumia watakaoshiriki Bata msituni Festival.

Tamasha la 'Bata Msituni Festival' ni sherehe ya kipekee ya Kiafrika inayolenga kuenzi na kukuza utalii wa mazingira na utamaduni, uzuri wa asili wa Afrika na Tanzania kwa ujumla, na watu wake kupitia utamaduni, sanaa na shughuli mbalimbali za burudani.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI