GRAND GALA KUNOGESHWA NA WAZIRI NDUMBARO SUPER DOM MASAKI

 


Wadau mbalimbali wa tansia ya muziki wa danzi wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 30 mwezi wa nane 2024, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Super dom bapo nyimbo mbalimbali zitapigwa za mziki wa zamani na kizazi kipya.

Aidha, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Damas Ndumbaro anatarajia kuwa mgeni Rasmi kwenye Tamasha la Gland Gala Dance lotakalofamyika Superdome Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es asalaam  Mkurugenzi wa Chocolate Princes Mboni Masimba ambaye ndiye mwandaaji wa tamasha hilo amesema kuwa siku hiyo itakua ni siku ya kipekee kwa wadau wa tansia hiyo kuweza kupata burudani mbalimbali.

Masimba amesema tamasha hilo litafanyika Agosti 30, Mwaka huu ambapo miongoni mwa wasanii watakaoburudisha ni Pacho Mwamba, Charlez Baba na wengine wengi.

Kwa upande wake Pacho Mwamba amewaita watu wengi kujitokeza kwenye Tamasha hilo wakiwemo wanamuziki wa Tanzania ili weweze kujifunza mengi ikiwemo namna ya kuimba "live".

Patcho Mwamba amesema atakuwepo msimu wa tatu wa uzinduzi wa tamasha la Grand Gala ambayo itafanyika 30,mwezi wa 8 ukumbi Masaki  ambapo wanamuziki wa kizamani na mziki wa kizazi kipya watakuwepo wanamuziki wengi ikiwemo Christian Bella, Pacho Mwamba.

Patcho Mwamba Lukusa ni miongoni mwa Wakongo walioteka tasnia ya burudani Bongo, akiwa ni muimbaji kutoka Kundi la CP Academia ‘Ngwasuma Full Dose’ ambalo zamani lilikuwa linajulikana kwa jina la FM Academia.

"Kama wewe kijana unapenda mziki njoo siku hiyo" Patcho Mwamba

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI