MAADHIMISHO YA SIKU YA HOMA YA INI KITAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu, HabariPlus
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Chalamila awataka wakazi wa Mkoa huo na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya homa ya Ini yatakayofanyika Julai 25 hadi 28,2024
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam RC Chalamila amesema mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya INI pamoja na Halmashauri zake tano na wadau mbalimbali wa maendeleo watafanya maadhimisho ya siku ya Homa ya INI kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika katika Mkoa huo.
Aidha RC Chalamila amesema maadhimisho hayo yanakusudia kutoa elimu na uelewa wa pamoja juu ya ugonjwa wa Homa ya INI pamoja na kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo huduma za Homa ya INI kama upimaji wa maambukizi ya virusi vya Homa ya INI, Chanjo za homa ya INI pamoja na huduma zingine za Afya na magonjwa mengine.
Hata hivyo, amesema katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya sinza darajani Halmashauri ya Ubungo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Ummy Mwalimu (MB) Waziri wa Afya.
Aidha, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa anaoufanya katika sekta ya Afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya na kwa Wakati" Nimalize kwa kusema ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mapambano ya Homa ya INI au Ni Wakati wa Vitendo" amesema Chalamila.
Comments
Post a Comment