NAIBU SPIKA WA BUNGE ZUNGU MGENI RASMI MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA FURAHIKA.

 

Na Mwandishi wetu, Habari Plus 

Naibu Spika la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu anatarajiwa kuwa mgeni ya rasmi katia mahafali ya 19 ya Chuo Cha Ufundi Stadi cha Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amewaomba wazazi na walezi wa vijana hao wanahitimu na wengine kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu katika maisha ya watoto wao.

Amesema kuwa, mahafali hayo yatafanyika Agosti 3 mwaka huu na wahitimu 120 wa kozi mbalimbali ikiwemo Ualimu, Sekretari, Hotel na nyinginezo ambazo zipo chini ya Veta na mhitimu ambaye amefanya vizuri kwa kila kozi atapewa zawadi kama ilivyo kawaida.

"Tunayofuraha kubwa  kwenda kusheherekea mahafari ya 19 tangu chuo hiki kianzishwe na mgeni wetu ataakuwa Mbunge wa Ilala, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mussa Zungu, hivyo tunawaomba wazazi ama walezi wa vijana ambao wanahitimu mafunzo haya waje kwa wingi kufurahia kwa pamoja na watoto kwa siku hii muhimu kwa maisha yao.

Ameongeza kuwa, mahafali hayo yanafungua milango kwa kundi lingine kujiunga na muhula mpya wa masomo kwa miezi sita na mwaka mmoja kwa kozi ya hoteli, Bandari na nyinginezo na tunawaomba vijana ambao wameishia darasa la saba, kidato cha pili ama kidato cha nne na wakashindwa kupata alama nzuri za kuendelea na masomo waje hapa kutimiza ndoto zao katika elimu.

Dkt Msuya ameongeza kuwa wanafunzi ambao wanajiunga na chuo hicho wanapata fursa ya kutafutiwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo na wale wanaofanya vizuri wanajiweka katika mazingira mazuri ya kupata ajira baada ya kumaliza masomo yao.

Amfafanua kuwa muhula mpya utaanza Septemba 10 mwaka huu pamoja na kozi mpya ya Uhariri na upigaji picha za video (Video Production) itaanza kufundishwa chuoni hapo jambo linalotanua wigo wa vijana wengi kutimiza ndoto zao kwa kupata ujuzi wa kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Amesisitiza kuwa yote yanafanyika kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua milango ya uwekezaji na kusababisha mashirika mengi kuja kusaidia vijana na wao kutoa elimu bure na jambo linalotakiwa sasa ni vijana kutumia fursa hiyo vizuri ili kujikomboa katika dimbwi la umasikini.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI