RC CHALAMILA AONGOZA KIKAO CHA BODI YA BARABARA NA KAMATI YA USHAURI YA MKOA

#Atoa maelekezo mahususi juu ya ufanisi na utekekelezaja wa miradi ya barabara katika Mkoa.

#Ataka kuwa na ubunifu wa matumizi ya ‘Road Reserve’ na maeneo ya wazi.

#Asema Dar es Salaam ni salama sana vitendo vichache vya kiharifu vimeendelea kudhibitiwa.






Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 24,2024 ameongoza kikao cha bodi ya barabara na Kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazi mmoja -Ilala.

RC Chalamila akiongoza kikao hicho alipata wasaa wa kusikia michango na ushauri kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho ambao ni waheshimiwa wabunge na wataalam wengine ambao walihudhuria kikao na baadaye Mhe Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wajumbe kulipatia suluhu tatizo la ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya barabara hususani ile ambayo tayari ilishatangazwa kutekelezwa, kwa hatua ya awali amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kuratibu timu ya watu wachache kwa ajili ya kwenda kumuona waziri mwenye dhamana.

Aidha RC Chalamila ameagiza kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha watu kuacha kujenga kwenye mabonde,na kuendelea kulinda kingo za mito kwa kupanda miti kandokando ya mito ambapo ameshauri ipandwe miti ya michikichi ambayo inapatikana Kigoma,hivyo katibu Tawala wa Mkoa alifanyie kazi jambo hilo

Vilevile RC Chalamila ameagiza kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo na maeneo ya ‘Road Reserve’ pamoja na ya wazi kuwe na ubunifu wa matumizi yenye tija na maslahi mapana kwa umma,pia wale ambao majengo yao yanaangalia barabarani washirikishwe kuweka perving na kupanda miti ya kuvutia ambayo italeta taswira nzuri ya Mkoa, hata hivyo kwenye suala la ubora na uwekaji wa viraka barabarani ameagiza kutekelezwa kwa wakati hususani zile sehemu zilizoharibiwa na mvua za El-Nino.

 

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema kwa upande wa ulinzi na usalama Mkoa uko shwari sana vitendo vichache vya kiharifu vimeendelea kudhibitiwa ambapo ametoa rai kwa kila mtu kuelimisha jamii kufuatia uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijami kuhusu kutekwa na ukatili dhidi ya watoto ni vizuri kutoa elimu ili kuondoa taharuki kwa jamii “suala la usalama ni jukumu letu sote tuendelee kushikamana” Alisema Chalamila.

Aidha kikao hicho kilihudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Viongozi wa chama Mkoa, TARURA, TANROAD, makatibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya wakuu wa Wilaya, Mameya, Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila na wataalamu wengine kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...