RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA KUWAENZI MASHUJAA
Na Mwandishi wetu, HabariPlus
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu katika jiji hilo, huku akiwataka kuwaenzi mashujaa wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa wa Tanzania katika eneo la mnara wa mashujaa mnazi Mmojq ilala jijini Dar es Salaam.
Aidha RC Chalamila amesema siku ya mashujaa ina umuhimu mkubwa katika historia ya Tanzania na kusema kuwa njia bora ya kuwaenzi mashujaa hao ni kuendelea kudumisha Amani na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.
Amesema kuwa, muasisi wa Taifa la Tanzania Hayyt Mwl Julius K Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayyat Abeid Karume hao wamekua mfano mzuri wa kuigwa kila inapoazimishwa siku ya mashujaa kwani amani iliyopo imetokana na misingi imara walioiweka.
"Kila ifikapo Julai 25 tunaadhimisha siku hii kwa kuwakumbuka wapigania uhuru mbalimbali wa taifa hili, wapo wengi ambao wengine wamekufa na wengine wapo hai wamefanya makubwa nchi hii "amesema RC Chalamila.
Ameongeza kuwa, wako mfano mzuri wa mashujaa walio hai ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni shujaa aliye hai kupitia kazi nzuri anayoifanya ndani ya Taifa hili ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika jamii kama vile SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na miradi mingine mingi ya Elimu na Afya.
Aidha, uhuru ulipo katika nchi hiyo ni ishara ya watu ambao wameacha alama kwa sababu ya uzalendo na ushajaa waliouonesha kwa kujitoa kwa nchi yao kuhakikisha inapata amani na inakua na uhuru ambapo mashujaa wengi wamerithi.
"Tunapozungumzia mashujaa tunapaswa kulinda na kuepuka na rushwa na fitna na yote yatakayopelekea kubomoka kwa jamii yetu tuendelee kulinda amani na kuenzi uhuru wetu"amesema Chalamila.
Amesema kuwa, Tanzania imepitia majaribu mengi kabla ya kupatikana kwa Uhuru na amani iliyopo sasa na kueleza kuwa Amani iliyopo ni matokeo ya kazi nzuri iliiyofanywa na mashujaa waliopoteza maisha pamoja na mashujaa waliohai ambao ni viongozi waliojitoa kuilinda na kusimamia amani ya nchi , hivyo ni muhimu kila mtu kuilinda amani.
Katika hatua nyengine Rc Chalamila amewataka watanzania kuendelea kuliombea taifa la Kenya kutokana na hali wanayopitia kwani ushajaa ni amani bila amani nchi haiwezi kuwa salama.
Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa Kitaifa yamefanyika katika Mkoa wa Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani ameongoza maadhimisho hayo.
Comments
Post a Comment