SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOTENDA UHALIFU, WAMO WANAOSAMBAZA JUMBE ZA UONGO WATOTO KUTEKWA

Na Mwandishi wetu, HabariPlus

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Serikali haikubaliani na vitendo vyote vya kihalifu wanavyofanyiwa baadhi ya watoto, huku akiahidi hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakaebainika kutenda vitendo hivyo.

Aidha, Serikali haitowafumbia macho baadhi ya watu wanaotumia fursa hiyo kusambaza jumbe za uongo kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mbaimbali na kuleta taharuki ndani ya jamii.

Kauli hiyo imetolewa jinini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamadi Masauni wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari alipokua akitoa taarifa ya matukio ya vitendo vya ukatili na utekaji wa watoto kwani sio tu vitendo viovu bali vinaenda kinyume na utamaduni wa Taifa lenye utu, ustaarabu, amani na utulivu.

Amesema kuwa, Serikali imechukua hatua stahiki kwa wale wote waliobainika na itaendelea kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuhusika na matukio hayo ya kihalifu, hivyo wanaungana na Rais Dkt Samia, wazazi na walezi kukemea vikali matukio hayo.

"Hatua kali zitachukiliwa kwa wale wote watakaobainika kuhusika na matukio haya ya  kihalifu na tunaungana na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia na watanzania wote wakiwemo wazazi na walezi kukemia vikali matukio haya ya kihalifu kwa watoto" amesema Mhandisi Masauni.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na Serikali hususani Jeshi la Polisi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa washukiwa wote wa vitendo vya kihalifu kwani wanaofanya matukio hayo wapo ndani ya jamii.

Sambamba na hayo amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya vyombo vya habari kuleta taaharuki kwa kutoa taarifa za uongo na ambazo zimeshatokea jambo ambalo sio sahihi.

Ameongeza kuwa, wataendelea kuaimarisha dori za mara kwa mara na kutoa kipaumbele kwa taarifa wezeshi toka kwa wananchi wema ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa haraka pale matukio hayo yanaporipotiwa kwa Jeshi la Polisi.

Hata hivyo amesema Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi na kwa kushirikiana na Wizara nyingine na Vyombo vya Dola imeweka mkakati madhubuti wa kuhusisha mambo mbalimbali ikiwemo kuongeza elimu kwa umma kuhusu utoaji wa malezi bora na ulinzi kwa watoto.

"Kwenye hili tutaongea nguvu zaidi kwa Polisi Kata nchi nzima na pia kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalumu na Wizara ya Katiba na Sheria kufikia na kutoa Elimu kwa wananchi kwa urahisi"amesisitiza Mhandisi Masauni.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI