SERIKALI YAAHIDI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WABUNIFU WA MAJENGO



Na Mwandishi wetu 

Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya ujenzi ili kutengeneza sheria ya ujenzi itakayosidia  wataalamu wa wabunifu majengo na wakadiriaji ujenzi AQRB kufikia matamanio ya kukuza sekta ya ujenzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi duniani.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Edward Mpogolo wakati akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Mashaka Biteko kwenye ufunguzi wa Mkutano wa  5 wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ambapo unafanyika kwa siku mbili.



Amesema kuwa, mkutano huo uwapeleke kwenye tafakuri ya kuangalia changamoto walizopitia kwa kipindi cha miaka 5 na kuzifanyia kazi katika maboresho ili kuweza kupiga hatua zaidi kama Taifa na kwenda mbele kwenye ubunifu zaidi.

Ameongeza kuwa, licha ya changamoto kubwa wanazozipitia lakini pia wameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kusajili wabunifu 1586 huku 33 ndio wakitoka nje.



Aidha, ametoa wito kwa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji  Majenzi (AQRB)wametakiwa kuwa wazalendo ili kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati miradi ya ujenzi wanayopatiwa na Serikali au sekta binafsi.

Hata hivyo, amesema kuwa baadhi ya wataalamu wa ubunifu wa majengo na ukadiriaji majenzi wamekua wakiangalia maisha yao binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha kwa muda mfupi huku suala la weledi kazini likiwa limewekwa pembeni hali ambayo inasababisha majengo kuwa chini ya kiwango.



"Jitihada zinazopatikana katika sekta ya ujenzi inatokana na nyinyi wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ukiona mafanikio yaliyopo kwa sasa yanatokana na nyinyi,hivyo kwa niaba ya serikali  nawaomba sana muwe Wazalendo ili tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan" amesema DC Mpogolo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TBA Dkt Daudi Kondoro amewapongeza watoa mada ambao wamechaguliwa katika mkutano huo kutokana na uzoefu wao ambapo watawapatia madam zenye welezi wahitimu ambapo watapatiwa mafunzo hayo.



Aidha, amesema watendaji wa wizara wataendelea kusimamisha sekta ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili waweze kua na weledi katika kazi zao.

"Wizara ya ujenzi itatenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo wataalamu 180 Kila Mwaka ambao wanahusika na bunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ili waweze kuwa na uelewa Moana katika taaluma yao" amesema Dkt.Kondoro.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi wa wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Dkt Ludigija Bulamile amesema kuwa miongoni mwa mada ambazo zitakazojadiliwa ni pamoja na mafunzo ya ubunifu wa kijani ambapo yamedhaminiwa na Wold benki (WB) .

Pamoja na muhtasari wa mpango mkakati wa wizara kuwawezesha wazawa ambapo makampuni ya ndani yachukue nafasi kubwa katika kusimamia miradi mikubwa inayotolewa na Serikali .

 "Utafiti wa vifaa vya ujenzi, mfumo wa ununuzi katika sekta ya ujenzi"

Mkutano huo wa tano wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi( AQRB) umeenda sambamba na mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo ya taaluma ya wabunifu Majengo na wadiriaji Majenzi ,ambapo zaidi ya wahitimu 130 wamepewa vyeti pamoja na muongozo utakaowasaidia kufanyia kazi.

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...