DIWANI LUCY LUGOME KUWAWEZESHA WANAWAKE KWA KUGAWA KUKU BURE
DIWANI wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome, amesema miongoni mwa mikakati yake ndani ya kata ya Kisukuru wilayani Ilala ni kuwawezesha kiuchumi Wanawake kupitia vikundi vyao kwa kugawa kuku bure 50 ili waweze kukuza mitaji yao kupitia vikundi .
Diwani Lucy Lugome, alisema hayo Dar es Salaam jana, katika mkutano wake wa wananchi ambapo mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, na mgeni Maalum Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto.
Wanawake wezangu wa Kusukuru kuna fursa inakuja kwa ajili ya kukuza uchumi kwa kushirikiana na wadau wangu wa Maendeleo hivyo kuna utaratibu maalum utawekwa, utaratibu kupitia vikundi vyenu muweze kupata kuku bure kupitia vikundi vyenu tuwawezeshe kiuchumi "alisema Lugome.
Diwani Lucy Lugome aliwataka wanawake wa Kisukuru kufuata utaratibu ili waweze kupata fursa hiyo kila mmoja kwani Kisukuru ya kisasa ya maendeleo inakuja .
Aliwataka wananchi, na wanawake wa Kisukuru kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za. Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuleta maendeleo ambapo kisukuru ya sasa imebadirika fursa za uchumi zinapatikana.
Akizungumzia miundombinu ya Barabara alisema barabara za kisasa zinazojengwa Kisukuru kwa kiwango cha lami,sekta ya afya Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imeshaekeza fedha kwa ajili kujenga hospitali ya kisasa yenye hadhi ya Rufaa
Alisema sekta ya afya eneo la hekari tatu kwa ajili ya ulipaji fidia shilingi milioni 353 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali lipo tayari ambapo zimetengwa shilingi bilioni 5 kwa ajili ya mradi huo.
Akizungumzia sekta ya Elimu alisema elimu sekondari kukamilika kwa madarasa matano fedha za UVIKO ,matundu ya vyoo,ununuzi wa madawati 590 na Elimu msingi vyumba vitano vya madarasa na uchimbaji kisima cha maji.
Comments
Post a Comment