CUF YATOA MSIMAMO WAKE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 202

 


Na Mwandishi Wetu, Dar 

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na mapendekezo kadhaa yaliyotolewa na vyama vya siasa ni vyema uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ungefanyika baada ya marekebisho ya Sheria na Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na upatikanaji wa Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa bila ya kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi ni ngumu sana haki kupatikana kwani waliokutana miaka minne imefika hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika, huku akitaka kuwepo na rasimu ya mabadiliko itakayojenga demokrasia .

"Katika kuadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi wadau wa siasa tulikutana pale Dodoma mwaka 2021  kila chama kilinaso sera zao huku wakitoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kupatikana kwa tume huru, katiba mpya, sheria ya vyama vya siasa ipitiwe upya pamoja na kuwepo kwa michakato shirikishi"

Amesema kuwa, uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na 2024  haukua huru wala haki, bali ulikua unyonyaji wa demokrasia, huku akitoa rai urudiwe, pia amesisitiza Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike baada ya marekebisho ya sheria.

Aidha, amesema Chama hicho  hakipo tayari kuungana na vyama vingine vya siasa ili kuing'oa  CCM, wala kuingia kwenye mtego wa mwaka 2015 kwani walipoteza viti vingi na kugeukana wao kwa wao  hivyo hatoshirikiana na chama chochote.

Prof Lipumba amesema uchaguzi wa mwaka 2015 waliamini kuwa wanaunganisha vyama kwa dhati, kumbe chama kingine kipo kimkakati kudhoofisha vingine kutokana na uchu wa madaraka.

"Wakati ule tulipokuwa UKAWA, nikiamini tuko pamoja wakati na narudisha fomu ya kugombea kiongozi mmoja wa chama (jina kapuni) ambaye tulikuwa naye katika muungano huo alikuja kuniwekea pingamizi dakika za mwisho jambo ambalo liliniumiza sana," amesema.

Pia aliongeza kuwa wakati wa ujazaji wa fomu kwa wagombea wa CUF, viongozi wa chama kingine (jina kapuni) waliwashawishi wajaze kama wanatoka kwenye vyama vyao na hiyo inadhihirisha walijipanga kudhoofisha vyama vingine.

Kulingana na changamoto hizo zilizojitokeza wakati huo wa kuunganisha vyama kwa lengo la kuwa na nguvu ya pamoja ili kuking’oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM), Prof Lipumba amesema kwa sasa wako ngangali na hawaofii kuunganisha vyama kikubwa wataongeza umakini.

Pia Prof Lipumba amesisitiza kwamba wakati Uchaguzi Mkuu ujao ukiwa umebakisha miezi michache kufanyika ni vizuri uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana ukarudiwa akimiani haukuwa huru na haki.

Wakati Prof Lipumba akitoa misimamo hiyo, pia amewaka wazi kuwa kwa sasa kamati ya chama hicho inayoshughulikia uwandaaji wa Ilani ya Uchaguzi inaendelea na mchakato huo kwa kutumia akili Mnemba (AI) ili kupata mawazo mapana ya kusaidia kufikia malengo stahiki.

"Kamati yetu inaandaa ilani ya uchaguzi kwa kutumia akili Mnemba na imani yetu itatatua changamoto mbalimbali zilizopo na kupata ilani iliyobora, pia watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa uchaguzi ni gharama, hivyo watuunge mkono kwa lengo la kuleta mabadiliko,"amesema.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...