BURAH KUIBADILISHA KIWALANI
Mgombea Udiwani wa Kata Kiwalani Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Iddi Bura amesema amejipanga kutatua changamoto zilizopo katika Kata hiyo ikiwemo miundombinu ya barabara hasa za ndani ya mitaa.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea barua ya uteuzi kutoka Kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Sylvester Yaredi ambapo amesema Serikali imeleta barabara za lami nyingi.
"Barabara za ndani ya mitaa bado ni changamoto mvua ikinyesha hazipitiki nitahakikisha natatua changamoto zote ikiwemo Afya elimu na Maji, nimejipanga kuwahudumia watu wa Kiwalani.
Amesema kuwa, Serikali imejitahidi sana kuleta barabara za lami lakini zile za mitaa ni korofi hasa wakati wa mvua, hazipitiki, amewahakikishia wananchi wa Kiwalani anaenda kuzitatua changamoto hizo.
"Kama ambayo Chama kimeniamini naomba na wananchi wawe na imani na mimi ili kuhakikisha Kiwalani inazidi kusonga mbele zaidi kwani tuna kwenda kufanya mageuzi makubwa katika sekta zote "
Kwa upande wa Changamoto ya ajira amesema anakwenda kutumia Viwanda vilivyopo katika Kata hiyo ili kuhakikisha anawasaidia vijana waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi na kuleta mageuzi makubwa ndani ya Kata hiyo.
Comments
Post a Comment